Njooni Mnazi Mmoja ulifahamu kiundani zao la Embe
 |
Maofisa wa Tanzania Agriculture Productive Program (TAPP) wakitoa maelezo kwa mgeni rasmi kuhusiana na namna wanavyofanya kazi |
 |
Alice Maro ofisa wa TAPP akifafanua jambo kwa mgeni rasmi |
 |
Add caption |
 |
Mkurugenzi wa Kilimo na Mazao wa Wizara ya Kilimo na Ushirika
Beatus Malema akisoma maelezo kutoka kwa mmoja kati ya woaneshaji wa embe |
 |
Ahhaa!acha nionje kwanza |
 |
Alipewa zawadi kutoka kwa Bakhresa ambao ni wadau wa embe |
 |
muda wa kuonja embe ndo huu |
 |
Hii juice we acha tu! yani ni tamu bila ya hata ya kuweka sukari |
 |
Kula embe mama |
 |
Timu kamili ya Kiladeda |
 |
Alifurahishwa na bidhaa za Bakhresa |
 |
Pia mgeni rasmi alionja juice |
WAKULIMA wa
zao la zmbe nchini wametakiwa kujikita zaidi katika kulima embe la kisasa ili
kuweza kumudu soko la nje ya nchi ambalo linazidi kukua siku hadi diku.
Wito huo
ulitolewa jana na Mkurugenzi wa Kilimo na Mazao wa Wizara ya Kilimo na Ushirika
Beatus Malema ambae alimwakilisha Waziri wa Wizara hiyo Christopher Chiza
katika ufunguzi wa maonesho ya siku tatu
ya kuonja embe.
Malema
alisema kuwa kwa sasa soko la embe katika anga la kimataifa ni kubwa na
kusisitiza kuwa wakulima wanatakiwa kupewa elimu na kuwezeshwa katika kujua
namna ya kulima embe ili kuweza kuuza nje ya nchi.
Alisema kuwa
serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa kilimo wataendelea na juhudi
za kutoa elimu na ruzuku kwa miradi mbalimbali yenye kulenga kuboresha zao
hilo.
Naye
Mwenyekito wa Chama Cha Wakulima wa Embe
nchini (Amagro) Burton Nsape alisema kuwa wakulima wengi wa zao hilo
wanazalisha maembe ya asili ambayo soko lake halipo nje ya nchi.
Alisema kuwa
chama chake kinaendelea na juhudi za kuhamasisha kwa kutoa elimu kwa wakulima
kutumia miche ya kisasa ambayo inazalisha maembe yenye kupata soko la nje ya
nchi.
Alisema kuwa
pia inawasaida wakulima katika kujua namna ya kutafuta masoko, kufunga vizuri
zao hilo, kuepuka wadudu waharibifu pamoja na mbinu nyingine za kisasa.
Akizungumza
na gazeti hili mmoja kati ya walioneshaji wa bidhaa za Embe katika maonesho,
Joseph Mallya wa shamba la Kiladada alisema kuwa wakulima wengi wa embe
wanakabiliwa na changamoto ya kupata masoko ya uhakika ya ndani.
“ Wakulima
tunajitaidi kufanya vema tunalima aina mbalimbali ya maembe kama vile Palmer,
Keitt, Tommy, Apple na mengineo lakini sasa kinachotakiwa kwa sasa ni
kuhakikisha kuwa tunapata masoko ya uhakika lanii hata hivyo tuinajitaidi
kufanikisha hilo” alisema Mallya.
Maonesho
hayo ya siku tatu yalianza jana na yanatarajia kumalizika kesho katika viwanja
vya Mnazi Mmoja ambapo kiingilio ni bure.
Mwisho
0 comments: