TOP NEWS

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Maecenas mattis nisi felis, vel ullamcorper dolor. Integer iaculis nisi id nisl porta vestibulum.

Tuesday 1 January 2013

BREAKNEWSSSS SAJUKI NO MORE

Msanii wa filamu nchini Sajuki amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu, alifariki jana katika hospitali ya taifa ya Muhimbili ambapo alikuwa amelazwa baada ya kusumbuliwa na saratani ya ngozi.

Sajukia atakumbukwa kwa kuwa ni mmoja kati ya wasanii wakubwa ambao wamekuwa wakijitaidi kwa kiasi kikubwa kuhakikisha wanainua tasnia ya filamu na wasanii wenyewe kwa ujumla.

Sajuki alikuwa ni msanii asiyekuwa na mikogo hata kidogo bali alikuwa ni msanii ambae alikuwa anania na shauku ya kuona kuwa wenzake wanakuwa na maendeleo katika tasnia ya filamu.

Akiwa mgonjwa aliwahi kupelekwa nchini India kwa matibabu zaidi kwa mchango wa wasanii pamoja na wapenzi wengine wa filamu nchini.

Blog hii kwa masikitiko makubwa inaungana na mkewe Wastara pamoja na wasanii kwa ujumla katika kipindi hiki kigumu.

Mengi tutaendelea kuwajuza kuhusiana na jembe hili la nguvu ambalo limetutoka ikiwa ni siku ya pili tu tangia kuuanza mwaka huu

0 comments: