Goldie Havery mchumba wa Prezoo afariki dunia
Goldie ndo huyo alikuwa hote lady kweli kweli |
MSANII
mahiri wa muziki wa kizazi kipya Ambwene Yesaya, AY, amesikitishwa na kifo cha
msanii mahiri wa nchini Nigeria Goldie Harvey ambae pia aliwahi kushiriki
katika shindano la Biog Brother Africa 2012
Goldie ambae
aliwahi kuimba wimbo uitwao Skibobo akishirikiana na AY ambapo wimbo huo uliweza kuanza kutimiza
ndoto za AY kuimba na wasanii wa Nigeria huku na msanii huyo ndio alikuwa ndio
msanii wa kwanza kutoka nchini Nigeria kuimbana AY.
AY
aliliambia gazeti hili kwa njia ya simu kuwa alikuwa akimkubali sana msanii
huyo kwa kuwa alikuwa ana ushirikiano mzuri na alikuwa na mapenzi na wasanii wa
Afrika Mashariki.
Alisema kuwa
alimfahamu Goldie kupitia msanii Prezoo wa nchini Kenya aliyekuwa na uhusiano
na Goldie, AY alisema kuwa Goldie alikuwa na ndoto kubwa na alikuwa tayari
ameanza kufanya kazi nae na walikuwa na malengo makubwa mengi zaidi.
“ Yani huku
alikuwa ni msanii wa karibu sana na wasanii wa Afrika Mashariki na hivyo pia
ilikuwa ndio nafasi za awali za kuanza kufanya kazi na mdau huyu nap engine
tungefika mbali zaidi” alisema AY.
Msanii huyo aliyejichukulia umaarufu pia katika ukanda huu
wa Afrika Mashariki kutokana na uhusiano wake wa kimapenzi na msanii Prezoo wa
nchini Kenya waliekutana katika shindano hilo la BBA 2012.
Goldie aliaga dunia mapema juzi ambapo kwa mujibu wa meneja
wake aitwae Keke Ogungbe alisema kuwa Goldie aliumwa sana kichwa na
wakampikimbiza hospitali ambapo alifariki dunia muda mfupi baada ya kuwasili
hopsitalini hapo.
Golidie aliwahi kusikika akihojiwa katika kituo kimoja cha Luninga hapa nchini akisifia
ukarimu na uwezo wa wasanii wa hapa nchini na kusisitiza kuwa angependa kufanya
kazi zaidi na wasanii wa hapa nchini.
Mwisho
0 comments: