Kundi la akinadada la The Trio kuendelea kusaidia jamii
KIONGOZI wa kundi la muziki la The Trio, Angela Karashani alisema kuwa kila msanii ana jukumu la kuihudumia jamii kwa hali na mali.
Angela
alisema kuwa kwa kuwa wanajamii ndio wadau wakubwa wa kazi zao za sanaa wakiwa
kama ndio wanunuzi wakubwa hivyo wasanii wanatakiwa kurudisha kidogo
walichopata kwa wanajamii hao.
" Hii
ni fursa kubwa kwa sisi kama wasanii kusikiliza na kujifunza mengi kutoka kwa
watoto hawa na hivyo hata baadae tunaweza kutengeneza nyimbo za kuwasaidia
watoto hawa" alisema Angela.
0 comments: