TOP NEWS

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Maecenas mattis nisi felis, vel ullamcorper dolor. Integer iaculis nisi id nisl porta vestibulum.

Saturday 21 December 2013

Jokate anatufundisha mengi wanawake























JINA la Jokate Mwegilo sio jina geni masikioni mwa watu wengi hasa wadau wa burudani, Mitindo na hata filamu.
Mwanadada huyu amekuwa akijihusisha na masuala mengi katika jamii na amekuwa akisisika hasa kwa mtazamo chanya.
Amekuwa akitumia muda mwingi katika kufanya mambo ambayo yanang'arisha nyota yake huku akitumia muda wake mwingi katika kufanya kazi.
Hivi majuzi alizindua huduma mpya ya kutoa ushauri katika masuala ya urembo kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno kwa njia ya simu.
Kurasa wa Nyota Jumapili ulifanya jitihada za kutaka kufahamu mengi kuhusiana na mwanadada huyo na kile kilichomsukuma hadi kuanzisha huduma hiyo.
Akizungumzia uamuzi wake wa kuanzisha huduma hiyo ambayo mteja anatakiwa kutuma neno Kidoti kwenda 15678 ,  anasema kuwa kuanzia mwaka jana alianzisha huduma ya nywele ya Kidoti ambayo ilikuwa na lengo la kuwarembesha wanadada.
Anasema kuwa yangia hapo aliendelea na biashara hiyo ambayo alisema kuwa imekuwa ikiendelea vema kwa kiasi kikubwa.
Anaongeza kuwa baada ya kuendelea na biashara hiyo kwa muda mrefu kukawa na changamoto kubwa kutoka kwa wanadada ambao walikuwa wakitaka kuelimishwa masuala ya urembo na hapo ndipo akaamua kuwafikia kwa kutoa huduma hiyo ya ushauri wa urembo wa njia ya meseji.
"Najua mimi mbali na kuwa mbunifu katika kufanya biashara zangu za kukuza maisha lakini pia najaribu kufanya kila niwezalo kuwafikia wadada wenzangu na kujadiliana na nao masuala mbalimbali kama hivi urembo"anasema Jokate.
Anaongeza kuwa kwake anatambua kuwa kila mwanamke anaweza kuwa mrembo kwa kuwa urembo unaweza kutengenezwa lakini kwa upande wa uzuri hicho ni kitu cha kuzaliwa nacho.

Lakini hata hivyo anaongeza kuwa urembo peke yake sio kila kitu kwa mwanamke ambapo anawaasa wanawake wenzake kujituma na kutumia ubunifu zaidi katika kusaka maendeleo pia.
Anaongeza kuwa maendeleo kwa mwanamke ndio yatamwezesha kujipatia mahitaji mengine yote muhimu ukiwamo urembo pia.
Anatolea mfano nafsi yake kwa kuanzisha biashara ya nywele za Kidoti ambazo zinauzwa sana katika maduka ya Kariakoo na pia mikoani zimekuwa zikichangamkiwa zaidi.
Katika kuthibitisha dhana nzima ya kutafuta maendeleo ya kimaisha Jokate amejiingiza kwenye filamu za Bongo Movies.
Kwa sasa ameshakamilisha filamu moja kaiwa na mwigizaji Jacob Steven, JB ambayo inaitwa Mke Salama ambayo mwakani inaingia sokoni.
Anasema kuwa filamu hiyo imegusia masuala mbalimbali ya kimaisha likiwamo suala ya mapenzi na mengineo.

Lakini pia ameimba wimbo mmoja na msanii Luci uitwao Kaka na Dada ambao unaendelea kutamba kwa sasa huku akiwa anamhusudu zaidi msanii Judith Wambura, Lady Jaydee, Ay na Mwana FA.
Akizungumzia mikakati yake zaidi kwenye filamu anasema kuwa anataka mwakani kutoa albamu yake ambayo inaendelea kupikwa kwa sasa.
Anasema kuwa anataka kuendelea kufanya vema katika muziki hasa kutokana na kuwa na kipaji cha kuimba kucheza muziki.
Anasema kuwa kwa sasa bado hajaanza kupokea shoo za muziki na anaongeza kuwa pindi akimaliza nyimbo zake ataanza kupokea shoo ndani na nje ya nchi.
Jokate ambae ni mrefu wa wastani, mweupe, mchangamfu anaonekana kuwa ni mdada mwenye mambo mangi kichwani mwake.
Kujihusisha kwa mambo mengi kwa muda mfupi imewafanya watu wahisi pengine hajitambui na hajui nini anachotaka kukifanya.
Akizungumzia hilo anasema kuwa anajua kila kile anachoamua kukifanya na anataka kutumia muda wake mwingi kama mwanadada kijana kujtuma zaidi kwa kipindi hiki katika kutafuta hela.
"Najua mimi sio mwanamke wa kutegemea kupewa mbali na kuwa mzuri nina jina kubwa lakini sipendi kabisa masuala ya kutegemea wanaume kunipatia hela au kunitunza hiyo mwiko kwangu"anasema Jokate.
Akilifafanua hilo la kutotegemea mwanaume kumsaidia katika kujitafutia maendeleo anafafanua kuwa kwa wadada wengi hasa wenye majina wanategemea kuwekwa mjini na wanaume zaidi.
Anaongeza kuwa kwa upande wake kwanza kwa sasa hana mpenzi na hatarajii kwa sasa ila anachokifanya kwa sasa ni kuhangaikia hela.
Anaongeza kuwa anataka mwaka ujao aongeze mtaji wa biashara zake hadi kufikia zaidi ya milioni 200.
"Naamini kuwa naweza, nitaweza na lazima niweze kufikia malengo yangu tena mimi kama mimi najua mimi sitaki umaarufu wa kijinga yani kujifanya nionekane wa maana kwa fedha za kupewa"Alisema Jokate.
Maisha ya Jokate katika elimu yake ni kwamba amefanya shahada ya Political Science na aliamua kuachana kujiendeleza katika masomo zaidi.
Anasema kuwa alikuwa ameanza masomo ya Shahada ya Uzamili lakini hata hivyo alilazimika kuahirisha baada ya kutingwa na mambo mengi.
Lakini hata hivyo anafafanua kuwa kwake anapenda kufanya yale ambayo moyo wake unaridhia na kuongeza kuwa hilo limekuwa likimsaidia kufanikiwa katika mengi.
Mwanadada huyu ambae anawapenda wanasiasa kama akina John Mnyika ambae ni Mbunge wa Jimbo na Ubungo pamoja na Zitto Kabwe, anasema kuwa anaipenda na kuichukia siasa.
Anapenda kula na kuimba pamoja na kukutana na watu wapya kila siku huku akipenda zaidi kufanya shughuli za kijamii.
Anawataka wasichana wenzake kujituma na kuepuka kutumiwa kwa mambo mbalimbali ambayo yanadharirisha utu wao.
Anampenda zaidi Rais Jakaya Kikwete ambapo hakusita kuisifia hotuba yake ya hivi karibuni aliyoitoa wakati wa maziko ya Rais wa kwanza mwafika wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.
Anasema kuwa imewaelewesha watu duniani nafasi ya Tanzania katika kukuza demokrasia barani Afrika.
Jokate ni mdogo wa Constantine Magavila mmoja kati ya vijana ambao wamekuwa wakizungumzia masuala mengi kuhusiana na maendeleo ya vijana.
Pia anae dada yake aitwae Dessy Deria, na mdogo wake Martn Kalikali.
Aliwahi kushika nafasi ya pili katika shindano la Miss Tanzania mwaka 2006 ambapo mwaka huo huo Wema Sepetu ndio aliibuka na ushindi wa taji hilo.
Mwisho 

0 comments: