TOP NEWS

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Maecenas mattis nisi felis, vel ullamcorper dolor. Integer iaculis nisi id nisl porta vestibulum.

Friday 13 December 2013

Onja ya Swahili Fashion 2013








Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imeahidi kuendelea kuwaunga mkono wanamitindo nchini na kuwasaidia kufikia malengo yao.

Akizungumzia ushiriki wa kampuni hiyo katika maonesho hayo,  Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya Umma na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Joseline Kamuhanda alisema kuwa  kampuni hiyo inatambua mchango wa tasnia ya ubunifu katika kuongeza ajira na kukabiliana na umaskini.

Alisema kuwa kwa kutambua hiyo kampuni ya Vodacom ambayo kwamuda mrefu imekuwa ikijikita katika kusaidia tasnia hiyo kwa mwka aujao imejipanga kuhakikisha kuwa inashiriki kikamilifu katika kusaidia shughuli mbalimbali za ubunifu.

Aliongeza kuwa kampuni hiyo itahakikisha kuwa inaimarisha elimu ya ujasiliamali kwa wabunifu ili kuwaongezea mwanga katika kazi zao.

Aliongeza kuwa kwa kutambua mchango wa tasnia hiyo katika kuimarisha utamaduni hasa ikizingatiwa kuwa mavazi mengine ni ya yanalenga kukuza utamaduni Vodacom itaendelea pia katika kudhamini maonesho mbalimbali."Najua ubunifu wa mavazi ni moja kati  ya kazi ambazo zinaweza kuitangza nchi kimataifa zaidi na sisi kama Vodacom Tanzania ni tumekuwa tukihamasisha maendeleo yenye tija ya namna hiyo  hivyo kwa kudhamini tasnia hii tutakuwa tuanongeza chachu ya kuwafnya wabunifu hawa kufika mbali zaiid"alisema Joselin.

Kwa upande wake mmoja kati ya wabunifu wa mavazi walioshiriki katika onesho hilo Zamda George wa lebo ya Zaidi Afrika alisema kuwa kwa maonesho ya mwaka huu yamekuwa na hamasa kubwa hasa kwa kuwakutanisha wabunifu wa Tanzania na wa nchi nyingine mbalimbali.

"Kwa mwaka huu ambapo nimeonesha nguo zangu kadhaa naona kuwa kwangu ilikuwa ni fursa pia ya kukutana na kujifunza kutoka kwa wenzangu"alisema Zamda.
Onesho la Swahili fashion mwaka hu lilifanyika kwa siku tatu na kuwakutanisha wabunifu zaidi ya 30 huku wengine wakiwa wametokea nchi za nje Afrika Mashariki na Afrika nzima kwa ujumla.
Mwisho

0 comments: