Madada kuna aina zaidi ya 50 za embe poa kwa msosi
Hapo kuna embe Alfons, embe Apple na nyingine kibaooo |
Watu wakaanza kuzionja kama kawa |
hawa ni wadau wa shamba la Kilodede |
Watu walinawishwa na kuonjeshwa embe hapohapo |
Mwenyekiti wa Chama Cha Wakulima wa Embe (Amagro) Burton
Nsape akizungumza kuhusiana na namna ambavyo chama chake kinawasaidia wakulima
wa embe kujipatia kipato kupitia zao hilo anasema kuwa Amagro hutoa elimu kwa
wanachama wake.
Nsape anasema kuwa wakulima
mbalimbali walikuwa wakilima na kuuza hadi nje ya nchi embe kw amuda mrefu
ambapo anafafanua kuwa ni biashara nzuri na yenye faida kubwa.
Anasema kuwa Amagro inaendeleza
harakati za kuwapatia wanachama wake elimu ya maarifa mbalimbal kuhusiana na
ukulima wa zao hilo kama vile namna ya kudhibiti wadudu waharibifu, namna ya
kufunga na kuhifadhi embe ikiwa pamoja na matumizi ya madawa na mbolea.
Anasema kuwa changamoto kubwa
inayowakabili wakulima wa embe ni ukosefu wa usafirishaji wa kitaalamu kutoka
mashambani hadi kuelekea kwenye soko kwa kuwa ili kuweza kuliweka embe katika
ubora wake kuna mengi zaidi ya kuyafuata.
Akizungumzia kuhusiana na
aina ya embe na ubora unaotakiwa katika soko la nje anasema kuwa kuna aina
zaidi ya 1000 ya embe duniani kote.
Anafafanua zaidi kuwa kwa
hapa nchini kwa muda mrefu tumekuwa tukilima embe za asili ambazo soko lake kwa
nje sio kubwa.
Anasema kuwa katika tani laki
3.72 za embe ambazo hupatikana hapa nchini takribani kila mwaka ni asilimia 10
tu ambazo ni embe za kisasa huku nyingi zikiwa ni zile za asili.
Anasema kuwa Amagro imeamua
kuwahamasisha wakulima ambao ni wanachama wake kuzalisha aina ya nne za embe
ambazo ni Apple, Keit, Muyuni na Alfonso.
Anasema kuwa angalau wakiwa
na aina hizo za embe wanaweza kuwa na uhakika wa kupeleka embe na kuuza nje ya
nchi kwa kuwa hizo ni moja kati ya aina za embe ambazo zinatakiwa zaidi nje.
0 comments: