TOP NEWS

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Maecenas mattis nisi felis, vel ullamcorper dolor. Integer iaculis nisi id nisl porta vestibulum.

Saturday 5 January 2013

Njooni Mnazi Mmoja ulifahamu kiundani zao la Embe

Maofisa wa Tanzania Agriculture Productive Program (TAPP) wakitoa maelezo kwa mgeni rasmi kuhusiana na namna wanavyofanya kazi 

Alice Maro ofisa wa TAPP akifafanua jambo kwa mgeni rasmi

Add caption

Mkurugenzi wa Kilimo na Mazao wa Wizara ya Kilimo na Ushirika Beatus Malema akisoma maelezo kutoka kwa mmoja kati ya woaneshaji wa embe

Ahhaa!acha nionje kwanza

Alipewa zawadi kutoka kwa Bakhresa ambao ni wadau wa embe

muda wa kuonja embe ndo huu

Hii juice we acha tu! yani ni tamu bila ya hata ya kuweka sukari

Kula embe mama

Timu kamili ya Kiladeda

Alifurahishwa na bidhaa za Bakhresa

Pia mgeni rasmi alionja juice


WAKULIMA wa zao la zmbe nchini wametakiwa kujikita zaidi katika kulima embe la kisasa ili kuweza kumudu soko la nje ya nchi ambalo linazidi kukua siku hadi diku.

Wito huo ulitolewa jana na Mkurugenzi wa Kilimo na Mazao wa Wizara ya Kilimo na Ushirika Beatus Malema ambae alimwakilisha Waziri wa Wizara hiyo Christopher Chiza katika ufunguzi wa  maonesho ya siku tatu ya kuonja embe.

Malema alisema kuwa kwa sasa soko la embe katika anga la kimataifa ni kubwa na kusisitiza kuwa wakulima wanatakiwa kupewa elimu na kuwezeshwa katika kujua namna ya kulima embe ili kuweza kuuza nje ya nchi.

Alisema kuwa serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa kilimo wataendelea na juhudi za kutoa elimu na ruzuku kwa miradi mbalimbali yenye kulenga kuboresha zao hilo.

Naye Mwenyekito wa Chama Cha Wakulima wa  Embe nchini (Amagro) Burton Nsape alisema kuwa wakulima wengi wa zao hilo wanazalisha maembe ya asili ambayo soko lake halipo nje ya nchi.

Alisema kuwa chama chake kinaendelea na juhudi za kuhamasisha kwa kutoa elimu kwa wakulima kutumia miche ya kisasa ambayo inazalisha maembe yenye kupata soko la nje ya nchi.

Alisema kuwa pia inawasaida wakulima katika kujua namna ya kutafuta masoko, kufunga vizuri zao hilo, kuepuka wadudu waharibifu pamoja na mbinu nyingine za kisasa.

Akizungumza na gazeti hili mmoja kati ya walioneshaji wa bidhaa za Embe katika maonesho, Joseph Mallya wa shamba la Kiladada alisema kuwa wakulima wengi wa embe wanakabiliwa na changamoto ya kupata masoko ya uhakika ya ndani.

“ Wakulima tunajitaidi kufanya vema tunalima aina mbalimbali ya maembe kama vile Palmer, Keitt, Tommy, Apple na mengineo lakini sasa kinachotakiwa kwa sasa ni kuhakikisha kuwa tunapata masoko ya uhakika lanii hata hivyo tuinajitaidi kufanikisha hilo” alisema Mallya.

Maonesho hayo ya siku tatu yalianza jana na yanatarajia kumalizika kesho katika viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo kiingilio ni bure.
Mwisho 

0 comments: