Mdada Maya atinga Dar, ahamasisha haki za wanawake kupitia muziki
Huyu ndo mdada aitwae Maya ni msanii kutoka nchini Marekani alikuja hapa nchini kuhamasisha masuala ya haki za wanawake |
Hawa ndo waandaaji wa onesho hilo Chedi Nguru na Gaidi kutoka kampuni ya MegaMark Entertainment |
Maya akiendeleza mzuka katika onesho hilo lililofanyika katika ukumbi wa Trinity
Hawa ni moja kati ya madiva waliojitokeza siku hiyo
Chedi akiwa nyuma ya Maya ambapo pia Chedi aliimba ikiwa ni kumpa suport Maya
Mkuu wa Mahusiano wa Ubalozi wa Marekani Dana Banks
Balozi wa Marekani Alphonso akimpongeza Maya baada ya onesho lake hilo
Dana Banks akifurahishwa na onesho la Maya ambalo lilikuwa kali sana
Wafanyakazi wa Ubalozi wa Marekani wakiwa wanashow some love kwa kamera yetu
Maya pia aliimba na wasanii wachanga waliojitokeza siku hiyo kuimba na kuonesha vipaji vyao.
Habari Kamili.
MSANII wa muziki ambae pia ni mwanaharakati wa haki za wanawake kutoka nchini Marekani Maya Acuzena juzi alifanya onesho la kuvutia lililobeba ujumbe wa kuhamasisha haki za wanawake.
Maya ambae yupo hapa nchini kwa uratibu wa kampuni ya Matangazo bna Burudani ya MegaMark ambayo imemleta msanii huyo hapa nchini kwa mara ya pili.
Onesho hilo la Maya lilifanyika katika ukumbi wa Trinity ambapo alikuwa akiimba muziki wa moja kwa moja (Live) huku akisaidiwa na bendi ya Wa Kwetu ambayo ilikuwa ikipiga vyombo mbalimbali vya muziki.
Maya alionesha uwezo wa hali ya juu katika kumiliki jukwaa, kuimba, kucheza huku akiwashirikisha kikamilifu wapenzi wa burudani waliohudhuria siku hiyo.
Maya alikuwa pia akitoa ujumbe kuhusiana na haki za wanawake na pia alitumia muda wake mwingi kuzungumza na washabiki wake siku hiyo huku akiwapatia nafasi wasanii chipukizi kuimba nae jukwaani.
Mmoja kati ya wasanii wa juu ambao nao waliweza kuonesha uwezo wa kuimba na kutumia jukwaa ni Linah Sanga wa Tanzania House of Talent (THT) ambae pia alimvutia Maya.
Maya akiwa hapa nchini ametembelea mashirika mbalimbali ya haki za wanawake, watoto pamoja na wadau wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini.
0 comments: