Wanawake wa Ecobank walivyoadhimisha siku ya wanawake duniani
Mwanaharakati wa masuala ya maendeleo ya vijana, wanawake na elimu Modesta Mahiga akitoa somo siku hiyoPia kulikuwa wafanyakazi wanaume na wanawake pia siku hiyo
Wadada wafanyakazi wa benki wakaserebuka na muziki mkali
Wafanyakazi wa Ecobank
Bi Modesta huyo mbele akiserebuka siku hiyo
Muzikii huoooo wadada wa benki wakacheza kwa sana tu
Mfanyakazi mdogo kuliko wote wa Ecobank akiserebuka siku hiyo
CEO wa Ecobank Enoch Osei-Safo akitosi na wageni
Mwenyekiti wa bodi ya Ecobank akizungumza yake
Bi Teddy Mapunda na Regina Mwalekwa
Mgeni rasmi akapewa tuzo yake siku hiyo kutambua mchango wake katika kusaidia wanawake.
Habari Kamili
Wanawake wa Ecobank katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani waliadhimisha siku hiyo kwa kukutana pamoja na kujadiliana masuala mbalimbali kuhusiana na namna ya kumwendeleza mwanamke.
Katika mjadala huo wwanaharakati Mjasiriamali hapa nchini Modesta Mahiga Mwenyekiti Mtendaji wa Proffesional Aproach Group ambapo aliwataka wanawake wenye mafanikio na wanaoshikilia nafasi za uongozi katika ofisi mbalimbali kuwaendeleza walio chini yao.
Modesta alisema hayo juzi wakati alipokuwa akizungumza kuhusiana na namna ambavyo wanawake wanaweza kujiimarisha katika ngazi za uongozi.
Alisema kuwa wanawake wenye madaraka wanatakiwa kutambua kuwa kwa kuwaendeleza wafanyakazi wa chini yao ndio wanakuwa wamejiimarisha zaidi katika nafasi zao hizo.
Alisema kuwa kwa kuwaendeleza na kuwasaidia wanawake wa chini yao wanakuwa wana uhakika kwa kupata watu wa kuwasaidia kazi iwapo wao wanakuwa hawapo kazini kwa dharura au likizo.
" Mimi najitolea mfano mimi mwenyewe kuwa kwa kipindi ambapo nakuwa sipo ofisini naweza kukuta kuwa kumbe wale niliowaacha nimewajengea misingi ya kujiamini na kufanya shughuli kama inavyotakiwa, sasa kama nisingekuwa nimefanya hivyo si ndio ningekuta kila kitu kimeharibika"alisema Modesta.
Katika hafla hiyo iliyoandaliwa na benki ya Ecobank pia wafanyakazi walipewa zawadi mbalimbali ambapo mwanadada Abellalulu Sultan pamoja na Catherine Uliwa walipewa zawadi kuwa wafanyakazi wadogo zaidi katika benki hiyo.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa benki ya Ecobank Enoch Osei-Safo alisema kuwa benki hiyo itaendelea kuwasaidia wanawake katika ngazi mbalimbali za uongozi katika benkiu hiyo.
Alisema kuwa kwa sasa asilimia 40 ya wafanyakazi ni wanawake na kuongeza kuwa bado kuna mikakati mingi ya kuwasaidia wanawake hao.
0 comments: