TOP NEWS

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Maecenas mattis nisi felis, vel ullamcorper dolor. Integer iaculis nisi id nisl porta vestibulum.

Tuesday, 19 March 2013

Mdada Nancy Sumari awafunda wadada wenzake kwa njia ya kitabu

                                               Faraja Kota aliwakuwapo kuhamasisha zaidi siku hiyo


                Professa Mwaikambo ambae ni smhsindi wa Tuzo ya Martin Luther King akipokea kitabu kutoka kwa Nancy

                                                    Nancy akihutubia siku hiyo
                                                     Mwanafunzi akiuliza swali

MLIMBWENDE wa Tanzania mwaka 2005 Nancy Sumari jana alizindua kitabu kiitwacho Nyota Yako alichokitunga mwenyewe chenye ujumbe wa kuwahamasisha wasichana masuala mbalimbali yanayowahusu ikiwa pamoja na kutoa ujumbe mbalimbali wenye kulenga kusaidia kuwaepusha na hatari mbalimbali.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa kitabu hicho Nancy alisema kuwa akiwa kama mlimbwende pia mwanaharakati wa haki za wasichana ameona kuwa kuna kila sababu ya kuzungumza na wasichana wa Tanzania nzima kwa njia hiyo.

Alisema kuwa kitabu hicho chenye kurasa 26 kinaelezea nafasi ya mwanamke katika jamii ya kitanzania, uwezo wa mtoto wa kike, Umuhimu wa namna ya kujithamini, kuweka malengo, ndoto na maazimio, kujiamini kujiendeleza kimalengo.

Katika uzinduzi huo uliohudhuriwa na wadau wengi wa elimu nchini pia uluhudhuirwa na mshindi wa Tuzo ya JMartin Luther King Esther Mwaikambo ambae pia mbali na kumpongeza Nancy aliwasihi wasichana wenye mafanikio nchini kuwa na shauku ya kuwasaidia wasichana wengine wenye kutaka kutumiza ndoto zao.


0 comments: