TOP NEWS

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Maecenas mattis nisi felis, vel ullamcorper dolor. Integer iaculis nisi id nisl porta vestibulum.

Thursday 16 May 2013

Ally Choki aikubali Kili Awards


MSANII wa muziki wa dansi nchini Ally Choki amepongeza utaratibu uliotumika kuchagua washiriki wanaowania tuzo za Kili 2013.

Choki ambae miaka iliyopita aliwahi kusema kuwa hataki kushirikishwa kabisa katika tuzo hizo kwa kuwa hakukubaliana na utaratibu uliokuwa ukitumika kuchagua washiriki

Akizungumza na kituo kimoja cha Radio Choki alisema kuwa awali walikuwa wakiwaweka katika kipengele kimoja wagombea ambao muziki wao ulikuwa hauendani.

" Kwa mwaka huu naona kuwa angalau kile nilichokuwa nikikipinga kimefanyiwa kazi kwa kuwa hata wagombea wamewekwa wale ambao wanaendana hasa katika kipengele cha muziki wa dansi" alisema Choki.

Alisema kuwa zamani aliwahi kuwekwa katika kipengele kimoja na wasanii kama vile Gurumo na wengineo ambao ni magwiji wa muziki huo.

Alisema kuwa kwa yeye kushindanishwa na watu kama hao ni kosa kwa kuwa wanawekwa kwenye kundi la watu ambao wote wanaimba muziki wa dansi kwa kuwa wanaimba kwa nyakati tofautitofauti.

Alisema kuwa bendi kama za Msondo na Sikinde wanaimba muziki wa dansi kwa kizazi ambacho ni tofauti na hiki cha akina Choki, Banza, Muumini na Khalid Chokoraa.
Hata hivyo alisema kuwa yupo tayari kushiriki michuano hiyo ya Kili iwapo utaratibu ukiendelea kuwa mzuri kama ulivyo sasa.
==============


0 comments: