TOP NEWS

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Maecenas mattis nisi felis, vel ullamcorper dolor. Integer iaculis nisi id nisl porta vestibulum.

Thursday 16 May 2013

Msanii Ommy Dimpoz mzee wa madada awahasa wasanii wakongwe

WASANII wa muziki wa kizazi kipya ambao wamekuwa wakiimba kwa muda mrefu wametakiwa kutokata tamaa ya kazi zao hata kama wamesota muda mrefu bila ya mafanikio.

Hayo yalisemwa na msanii Omary Nyembo, Ommy Dimpoz, ambapo alisema kuwa anasikitishwa na wasanii kama hao ambao kwa sasa wanashinda wakilalama tu kuwa hawana bahati.

Alisema kuwa wasanii kama hao wanakuwa hawajisikii vema kuona kuwa kuna wasanii wapya wanakuja katika fani ya muziki na kuwakuta na kisha kuwaacha.

Alisema kuwa kawaida muziki una wakati na iwapo msanii wakati wake ukifika ndio anatakiwa kuutumia vema kujiimarisha katika soko.

" Mimi nashangaa sana  utakuta mtu msnaii lakini katika mazungumzo yake anakuwa haishi kulalama kuwa mara hoo wao hawatoka na mengine mengi inachotakiwa ni kujipanga sio lawana" alisema Ommy Dimpoz.

Kwa sasa Ommy Dimpoz ni mmoja kati ya wasanii wachache waliopo kwenye chati ya muziki wa kizazi kipya hapa nchini.

Msanii huyo amechaguliwa kugombea tuzo sita katika mashindano ya Kili Music kwa mwaka huu ambapo ameongoza kuwa msanii aliyechaguliwa katika tuzo nyingi.

0 comments: