TOP NEWS

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Maecenas mattis nisi felis, vel ullamcorper dolor. Integer iaculis nisi id nisl porta vestibulum.

Tuesday 14 May 2013

Sina Bifu na dingi wangu-- Q chief


MSANII wa muziki wa kizazi kipya Q Chilla amekanusha kuendelea kwa ugomvi dhidi ya baba  yake mzazi.

Q Chief alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati akifanya onesho lake katika klabu ya maisha.

Alisema kwa awalia alikuwa katika mzozo na mzazi wake huyo lakini kwa sasa hana tatizo nae tena.

" Kama mnakumbuka hata zile nyimbo zangu za mwanzo nilikuwa ninaziimbaje yani nilikuwa ni kama vile kuna vijembe fulani lakini kwa sasa mambo yangu na mzazi wangu huyu ni mazuri sana tu"alisema Q Chief.

Naye mzazi huyo akizungumzia muziki wa Q Chief alimtaka aimbe na kufika kiwango cha kimataifa.

Alisema kuwa anaipenda kazi ya mtoto wake huyo na imemsaidia kufikia malengo yake mbalimbali na hakusita kumwagia baraka zake Q Chief.

" Mimi kama mzazi namtakia maisha mema kijana wangu huyu ili afike katika ngazi za kimataifa kwa kuwa uwezo anao na kila sababu ya kufanya hivyo ipo"alisema mzazi wa Chief.

0 comments: