TOP NEWS

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Maecenas mattis nisi felis, vel ullamcorper dolor. Integer iaculis nisi id nisl porta vestibulum.

Monday 13 May 2013

Mbunifu Doreen wa Escardo alonga kuhusiana na wasanii na mavazi


   
MBUNIFU wa mavazi mahiri nchini anayetamba na lebo yake ya Eskardo  Bird aitwae Doreen Noni kwa sasa awasisitizia wasanii kuwa na wabunifu wao wa mavazi pia.

Doreen ambae pia ni mtaalamu wa masuala ya upangiliaji wa mavazi amehusika kwenye kuwapangia mavazi wasanii wanaoshiriki kwenye mchezo wa kuigiza wa Siri ya Mtungi.

Doreen pia alihusika kwenye kuwavalisha washiriki wa shindano la Epi Bongo Star Search kwa mwaka 2012.

Mwanadada huyo alisema kuwa wasanii mbali na kuwa ni kioo cha jamii lakini pia wanatakiwa kujitambua kuwa mavazi yanaweza kuwaongezea umahiri katika kazi zao.

Alisema kuwa iwapo wasanii wakitambua nafasi ya mavazi katika kuimarisha haiba yao kisanii hawatasita kuwatumia wataalamu wa mavazi katika kuwapangia kuvaa.

" Naona kuwa wasanii wa hapa nyumbani wakijipanga na kutumia ghara ma kidogo katika kupanga mavazi basi watakuwa wamefanya kitu muhimu kwa kuwa nafasi ya mavazi ni kubwa katika kazi za sanaa hapa nchini" alisema Doreen.

0 comments: