Ni muhimu kuisoma hii
Na Evance Ng'ingo
KAMA ikiulizwa moja kati ya taarifa za habari za
burudani na sanaa ambazo zilitawala katik avyombo vya habari mbalimbali hapa
nchini kwa siku kadhaaa zilizopita basi ni mzozo kati ya msanii wa muziki za
kizazi kipya Judith Wambura na Kituo cha Clouds FM.
Sakata hilo lililodumu kwa muda wa siku kadhaa ambapo
upande mmoja ulikuwa ukishambulia zaidi na hadi upande wa pili wa Clouds Media
ulipoamua kulitolea ufafanuzi suala hilo.
Yapo mengi ya kujifunza na ambayo wasanii kwa ujumla
wanatakiwa kujifunza katika kipindi hiki cha siku hizo ambazo yalikuwapo hayo
malumbano.
Zipo hoja nyingi ambazo zilitolewa na Lady Jaydee
ambapo moja kati ya hoja kubwa aliyokuwa akiilalamikia ni kuhujumiwa kwa nyimbo
zake kutochezwa katika kituo hicho cha Radio.
Hiyo ilikuwa ni ndio hoja kubwa zaidi ambayo ilipelekea
kwa msanii huyo kujikuta akisisitiza kuwa hata akifariki dunia baso viongozi wa
kituo hicho ambayo ni Joseph Kusaga ambae ni Mkurugenzi Mtendaji pamoja na
Rugemalila Mutahaba ambae ni Mkurugenzi wa utafiti wasifike kwenye maziko yake.
Binafsi naona kuwa kwa hoja kama hiyo na nyinginezo
zinanipatia picha kuwa wasanii wengi wamekuwa na mtazamo wa kufikiria zaidi
nyimbo zao kufahamika kupitia radio zaidi.
Nikisema kuwa wasanii wanatakiwa kuw ana mengi ya
kujifunza ni hasa katika kuangalia njia mbadala za kuhajkikisha kuwa nyimbo zao
zinasikika hata bila ya kuwepo kwa radio.
Nampongeza Jide kwa kuhakikisha kuwa ameamua kuuza
albamu yake kwa njia za kisasa kabisa ambapo anawatumia wauzaji wa mtandao wa
Max Malipo ambapo albamu yake nzima itakuwa ikiuzwa.
Umakini kama huo katika ubunifu ni umakini ambao
unatakiwa kutumika katika kuzitangaza nyimbo zake pamoja na kuhimili ushindani
wa aina mbalimbali.
Kwa msanii mkubwa kama yeye sio kitu cha kuwafurahisha
wapenzi wake wa burudani kusikia kuwa analalamikia nyimbo zake kutochezwa na
kituo kimoja cha radio.
Ikifika wakati msanii akajiingiza katika malumbano kama
hayo ni dhahiri kuwa hata wapenzi wake wa muziki nao wanakuwa ni kama wapo njia
panda kwa kuwa sio wanachotakiwa kukisikia kwa muda huu wa matayarisho ya
uzinduzi wa albamu.
Suala la nyimbo za wasanii kutochezwa kwenye vituo vya
radio sio geni kwa kuwa wasanaii wengi ambao nao pia walijikuta nyimbo zao
hazichezwi radioni kwa sababu mbalimbali.
TID ni mmoja kati ya wasanii ambao nyimbo zao ziliwahi
kupigwa marufuku kuchezwa kwenye kituo cha Clouds na lakini hata hivyo aliweza
kumaliza sakataka hilo.
Msanii Rehema Chalamila, Ray C nyimbo zake ziliwahi
kuzuiliwa kuchezwa kwenye kituo cha East Africa Radio hadi alipoomba msamaha na
hata kwa sasa Diamond nae amekuwa kwenye sakata kama hilo pia kwa radio ya
Magic Fm.
Hivyo kukataliwa msanii kuchezwa nyimbo zake sio geni
kwa sekta hiyo ya sanaa hapa nchini lakini hata hivyo suala linabakia kuwa ni
haki kutochezwa nyimbo zao redioni.
Rugemalila Mutahaba analizungumzia suala hilo kuwa hata
msanii mahiri wa muziki wa Marekani Kanye
West alipokosea katika tuzo za MTV kituo hicho cha Luninga kilikataa kucheza
nyimbo zake kwa muda.
" Ikumbukwe kuwa hivi ni vituo binafsi vya Radio
na iwapo mtu akikosea basi au akifanya mambo ya utovu wa nidhamu ipo haki ya
kuadhibiwa kwa namna mbalimbali, sisi kama Clouds nyimbo za Jide tumezicheza
mara nyingi sana tu lakini amekuwa akitukejeli katika mitandao ya kijamii na kwengineo"
anasema Ruge.
Anafafanua kuwa "kituo hiki kimeamua kuacha
kutumia nyimbo za msanii huyo kwa kuwa hata mwenyewe alisema kuwa ana mpango wa
kufungau kituo chake cha radio na alisema kuwa hana haja ya nyimbo zake
kuchezwa huku kwetu, sasa sisi tumazimishe ya nini".
Nikisema kuwa yapo mengi ya wasanii kujifunza ni moja
kuhakikisha kuwa watafute wataalamu watakaowawezesha kujua namna ya kuzitangaza
nyimbo zao hata kwa kutumia blogs, tovuti na kwengineko.
Hapa pia linakuja suala la umuhimu wa kuwa na wataalamu
katika masuala ya Utawala wa Sanaa (Art Management), kama wakiwepo hao sio
rahisi kwa msani kujikuta akiiingia katika marumbano au mtafaruku wa aina
yoyote ile ya sanaa.
Huenda hata hili la Jide lisingefikia hatua kama hiyo
iliyofikia ya hadi watu kutukanana katika mitandao ya kijamii.
Au huenda kuna ukweli kuwa eti Jide ameshindwa kuhimiri
ushindani ambao kwa sasa unamkabili hususan ujio wa bendi ya Skylight
iliyochukua wasanii wengi kutoka kwenye bendi yake ya machozi.
Kwa sasa bendi hiyo ina wateja wengi zaidi huku wakiwa
na mikakati mizuri ya kutumia fursa za kujitangaza zilizopo kuanzia katika
radio, blogs na magazeti.
Kwa sasa bendi hiyo ambayo haina wasanii wenye majina
makubwa sana lakini ndio katika hafla mbalimbali na hata shoo zao wamekuwa
wakipata watu wengi.
Iwapo hiyo ni moja kati ya sababu za mjadala wote huo
nandio ukapelekea kuwatolea maneno wamiliki wa kituo hicho basi ni vema hapa
ukatumika zaidi ule ueledi wa masuala ya Arts Management.
Hapa nikiwa na maana ya kuwa jaribu kujisoma na
kuangalia futrsa iliyopo katika kujitanua zaidi na kuuhimili ushindani.
Jina lako ni kubwa na wewe unaweza kujipanga na
kuendelea kuwa na wateja wako kama kawaida sasa kama wakati upo na waimbaji
kama Sam Machoz, Mwinyi na wengineo ulikuwa unaweza panda jukwaani kuanzia saa
sita au saba sasa anza mapema zaidi.
Usibakie kuwa muimbaji bali pia ingia kwenye hatua ya
uburudishaji zaidi kwa kucheza na kuimba ili kuwafurahisha zaidi wateja wako.
Gadner Habash ambae ni Meneja wa Jide anasema kuwa kwa sasa
msanii huyo anakuja na staili mpya ambazo pia zitaendeelea kumweka kwenye
chati.
Hatua hiyo ni muhimu kwa kuwa hata kama wapo wasanii
ambao waliamua kurudi na kuomba suluhu kwenye vituo vya radio
walivyokorofishana navyo.
Kwa sasa wapo wadau mbalimbali ambao wanashauku ya
kuendelea kuzisikia nyimbo za Jide katika radio hiyo
Mmoja kati ya wadau hao ni naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na
Michezo, Amos Makalla ambae amejitokeza wazi na kutaka kuwepo kwa suluhu.
Anasema kuwa yupo tayari kukutana na pande hizo mbili
kusaka suluhu la kudumu la mgogoro huo, akisema malumbano hayana tija na
yanakuza mgogoro.
“Kutokana na malumbano ya Jide (jina jingine la Jaydee)
na uongozi wa Clouds, natoa mwito nikutane na pande mbili. Nawasihi sana
malumbano hata hayatakuwa na tija, bali kukuza mgogoro uliopo sasa,” alisema
Naibu Waziri Makalla.
“Sifurahi hata
kidogo jambo hili linaloendelea halijengi. Nimsihi sana mdogo wangu na shemeji
yangu Jide, akubali tukae pamoja na niwaombe Clouds wakubali tukae pamoja.
Naamini tukikaa pamoja tutaongea jambo hili litakwisha,” alisema Makalla.
Hata hivyo huenda hatua hiyo ya makala ikatatua mgogoro
huo na kujikuta wapenzi wa Jide wakiendelea kuzikisikia nyimbo zake kituoni
hapo kwa kuwa hata Ruge aliwahi kumsihi Jide atafute watu anaowaamini ili
wawasikilize pande zote mbili na kutafuta muafaka.
Mwisho
0 comments: