MSHIRIKI
wa shindano la uimbaji la X Factor Gamu Nhengu amesema kuwa hata akipata nafasi
ya kuimba kwa mara ya pili katika shindano hilo hatoweza kufanya hivyo.
Gamu
alitolewa katika shindano la mwaka 2010 na jaji was shindano hilo Cheryl Cole
baada ya kushawishiwa na Cher Llyod.
Gamu ambae ni raia wa nchini
Zimbabwe yeye pamoja na familia yake walituhumiwa kujihuisha na masuala ya
ubadhirifu na kisha wakatishiwa kurudishwa nchini mwao kutoka Uingereza.
Lakini hata hivyo baadae aliruhusiwa
kuendelea kuishi nchini humo kwa sasa amekuwa akitumikia mkataba wake wa kuimba
kwa miaka miwili akiwa anaandaa albamu yake ya A Love Like This.
Alisema kuwa " hata leo hii nikitapa
nafasi ya kufanya vitu vyangu katika onesho hilo sijui yani hata itakuwaje kwa
kuwa sina mzuka tena" alisema Gamu.
Kwa sasa anatamba na wimbo wa A Love
Like This uliobeba jina la albamu hiyo pia anatarajia kuachia wimbo mwingine.
Alionesha kuishukru studio aliyoiita
kuwa ni ndoto iliyopo nchini Scotland na kuongeza kuwa imemsaidia kurekodi
wimbo huo mmoja ambao anasema kuwa asingeweza kufanya hivyo iwapo angeshinda
shoo ya X Factor.
|
0 comments: