Chris Brown na Rihana, we acha tu!
LILE sakata la kuachana kwa wasanii
mahiri wa muziki wa kisasa nchini Marekani Chris Brown and Rihana waliokuw ana
uhusiano wa kimapenzi kwa sasa
limechukua sura mpya baada ya kudhihakina kwenye mtandao wa kijamii wa
twitter.
Katika kuonesha kuwa anamtupia
kijembe mpenziwe huyo ambae kwa sasa sio wake tena Rihana aliandika kwenye
akaunti yake ya twitter kuwa ana kitu
kwa ajili ya watu wa zima na kusisitiza kuwa Brown sio mtu mzima.
Hoja hiyo ilionekana kuwagusa wengi
ambao kwa sasa wanaonekana kuwa wamekuwa wakifuatilia ugomvi wao huo kwa muda
mrefu.
Utata huo ulianzia zaidi Jumatano
iliyopita ambapo Chris Brown aliandika kwenye akaunti yake ya twitter kuwa
hawezi kufikiria kuwa kuoa mtu ambae bado ni mtoto.
Hapo hapo Rihana naye alijibu kuwa
hana mpango wa kujiweka zaidi ya kuzingatia kuwa na heshima, upendo na
hadhi kwa asilimia 100 na mapenzi sio
kwa ajili ya watoto.
Wasanii hao walihi kuwa na uhusiano
wa kimapenzi kabla ya kutengana ambapo Chris Brown aliwahi kuamriwa na mahakam
kuwa asimsogelee msichana huyo kutokana na kitendo cha kimpiga.
Hivi karibuni walirudiana tena na
kuwa katika uhusiano ambapo haukudumu kama ule wa awali na kwa sasa wametengana
tena.
Rihana alionekana mitaa ya New York akidhurura
na ambapo inasemekana kuwa amerejesha uhusiano wake na JR Smith aliyekuwa
mpenzi wake na akijibu hilo Chris Brown alisema kuwa Rihana kuwa sio wake ila
ni wa mtu mwingine kwa sasa.
Hata hivyo kijana huyo alimwalika
mpenziwe wa zamani Karrueche Tran kwenye sherehe yake ya kuzaliwa muda mfupi
kabla ya kuzungumzia kuvunjika kwa uhusiano wake na Rihana.
0 comments: