Utoto wa Justin Bieber waacha gumzo Dubai
Baada ya kukumbana na kisanga cha kupigwa akiwa
nchini Dubai mwanamuziki kijana mwenye
mafanikio makubwa wa raia wa Marekani Justin Bieber huenda akajikut akihojiwa na Polisi wa
nchini humo.
Hiyo ni kufuatia kitendo cha kuendesha gari la
kukodi kwa mwendo kasi huku vinasa mwendo vya nchini humo vikishindwa kurekodi
mwendo kasi alikuwa nao kwa wakati huo.
Akiwa kwenye gari hilo la kifahari la mwendo kasi
kijana huyo alikuwa akiendesha gari hilo kwenye barabara ambayo inaaminika kuwa
na vinasa mwendo sita lakini cha hajabu hakuna kilichorekodi mwendo wa gari
hilo alilokuwa akiliendesha.
Shuhuda wa tukio hilo Nikki Jameson alisema
kuwa Bieber alikuwa akiendesha kwenye mtaa wa Sheikh Zayed Road ambapo karibia
kila kamera ilizima muda huo wakati alipopita.
Lakini hata hivyo kun akamera
iliyomuonesha akiwa ametokeza kichwa nje karibia nabasi alilopishana nalo
wakati akiendesha gazri lake hilo la kifahari.
Justin Bieber alikuwa akiendesha
gari hilo la kukodi lenye thamani ya pauni 12,000 kutoka kwenye hoteli ya
kifahari ya Burj Al Arab Hotel kuelekea kwenye uwanja wa e Sevens Stadium.
"Huyu yani kwanza bado
anahitaji miaka mingine kama miwili hivi ndio aruhusiwe kukodisha gari la aina
hiyo katika nchi hii hivyo anaweza kuhojiwa na Polis kuhusiana na sakata hilo
zima" alisema shuhuda huyo.
Katika mtiririko mzima wa maonesho
ya muziki nchini humo Bieber alichelewa kuanza kwa moja ya onesho lake nchini
humo ambapo aliwasiri jukwaani saa mbili baada ya muda wa shoo kuanza na
alishidnwa kuomba msamaha kwa hilo.
0 comments: