TOP NEWS

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Maecenas mattis nisi felis, vel ullamcorper dolor. Integer iaculis nisi id nisl porta vestibulum.

Sunday 7 July 2013

Jay Z amuibua mdada huyu



BAADA ya kuvivumbua na kuviendeleza vipaji vya wasanii kama vile Rihanna na Rita Ora msanii mahiri wa Hip Hop Jay-Z kwa sasa anaingia katika harakati za kumuendeleza msichana mdogo katika tasnia ya utayarishaji wa muziki.

Kwa sasa Jiga kama anavyofahamika na watu wengi amemchukua msichana wa miaka 16 raia wa nchini Kanada aitwaye  Ebony  Oshunrinde aka WONDAGURL kutayarisha iitwayo  Magna Carta Holy Grail.

Mwanadada huyo alipata bahati hiyo ya kuitwa kwenye dili hilo kufuatia rafiki yake ambae pia anafahamiana na Jay Z.

Kwa sasa ameujnganishwa kwenye dili hilo ambalo linatarajia kukamilika Almamis ijayo na litashirikisha kampuni ya simu ya Sumsung.

Dili hilo linampatia fursa mwanadada huyo kujiingizia fdha nyingi katika  kutayarisha albamu hiyo ambapo pia anaweza kujikuta akijitengenezea mazingira ya kula feda hizo kirahisi zaidi.

Rafiki huyo wa Jiga itwae Bling king alisema kuwa amefurahishwa n auwezo wa mwanadasa huyo wa kutayarisha muziki na kuongeza kuwa anaweza kuwa mtayarishaji bora wa baadae.

Kwa upande wake mwanadada huyo alisema kuwa kwa upande wake anaona kuwa hiyo ni fursa kubwa kwa kuonesha ulimwengu kuwa hata wadogo wanaweza kufanya mambo makubwa kwenye muziki.

Pia mwanadada huyo aliwahi kutengeneza beat kwa kutumia laptop yake na kuituma kwa rafiki wa karibu aitwae Travis Scott anaefanya kazi kwa ukaribu zaidi na Kanye West pamoja na  Jay Z beat hiyo ilikuw ana maadhi ya Raggae.

Mwanadada huyo wa miaka 16 alisema kuwa alipigiwa simu na rafiki yake huyo akimwambia kuwa anakaribia kuyabadilisha maisha yake hali ambayo alisema kuwa kwake alikuwa akiona kuwa ni kama ndoto.

 “Kwa sasa najua kuwa watu wengi wanataka kufanya kazi na mimi na huu kwangu naona kuwa ndio mwanzo wa mafanikio kwangu najisiki furaha sana" alisema mwanadada huyo.

Ebony anaungana na wanadada wengine kama vile Rihanna na Rita Ora ambao wote waligunduliwa na kuendelezwa vipaji vyao na Jay Z.



0 comments: